29.9 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

LAMAR: WINGI WA STUDIO HAUNITISHI

Na LUCY SAID (TURDARCO)

MTAYARISHAJI wa muziki kutoka studio ya Fish crab, maarufu kwa jina la Lamar, amesema uwepo wa studio nyingi nchini haumtishi kwa kuwa uwezo wake bado ni mkubwa japokuwa yupo kimya.

Akizungumza na MTANZANIA jana, alisema wasanii wengi hapa nchini wamefungua studio kwa ajili ya kufanya kazi zao pamoja na kazi za watu wengine, tofauti na miaka iliyopita na ushindani ulikuwa mdogo.

“Uwepo wa studio nyingi  haunitishi na hauniathiri kwa kuwa kinachohitajika ni ujuzi na uwezo wa kufanya kazi hiyo. “Msanii daima atabaki kuwa msanii na huwezi kumlinganisha na prodyuza kwani wana ujuzi tofauti japo ni mara chache sana kwa msanii kuwa prodyuza, lakini prodyuza kuwa msanii inawezekana.

“Kikubwa ni uwezo, nina taaluma ya maandalizi ya muziki hivyo sina wasiwasi na wingi wa studio, bado uwezo wangu upo pale pale,” alisema Lamar.

Lamar aliongeza kwa kusema ameamua kuweka muziki kando kwa muda ili kuendeleza biashara zake kama vile ‘Car wash’ na vitu vingi vinavyohusu magari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles