27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Lahm anogewa na Guardiola

Fussball  1. Bundesliga Saison 2013/2014: FC Bayern Muenchen - Borussia MoenchengladbachMUNICH, Ujerumani

NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm, amemtaka kocha wa klabu hiyo, Mhispania Pep Guardiola, aongeze mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi hicho.

Lahm alikuwa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kilichoibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Cologne katika mchezo wa Bundersliga uliopigwa kwenye dimba la Allianz Arena mwishoni mwa wiki iliyopita.

Mkataba wa Guardiola na Bayern utamalizika mwakani, huku kocha huyo akiwa kimya juu ya mustakabali wake baada ya kumalizika kwa mkataba huo, lakini Lahm anaamini kuwa wachezaji wa timu hiyo wanavutiwa na uwepo wa kocha huyo klabuni hapo.

“Maoni ya timu yapo wazi. Tunafurahia kufanya kazi tukiwa na Guardiola na ni kocha mwenye msimamo. Ingawa hatufanyi maamuzi, ninachoweza kusema ni kwamba timu ingependa kuona Guardiola akibaki. Tayari nimeshamwambia Guardiola kuhusu hilo,” alisema nyota huyo.

Guardiola, ambaye aliwahi kukinoa kikosi cha Barcelona ya nchini Hispania, ameisaidia Bayern kushinda vikombe viwili vya Bundersliga tangu atue mwaka 2013.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles