Diego Costa: Mimi si malaika

0
685

diego-costaLONDON, England

MSHAMBULIAJI wa timu ya Chelsea, Diego Costa, amesema anajua kwamba yeye si malaika uwanjani na kwamba hatabadilisha mtindo wake wa uchezaji soka.

Costa amepigwa marufuku mechi tatu mara mbili mwaka huu, mara ya kwanza kwa kumkanyaga mchezaji wa Liverpool, Emre Can na mara ya pili kwa kumsukuma beki  wa Arsenal, Laurent Koscielny.

“Nimefika mbali hivi kutokana na jinsi ninavyocheza,” mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwaambia waandishi wa habari.

“Sitabadilisha hilo eti kwa sababu ya vile watu wanavyochukulia uchezaji wangu,” aliongeza staa huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here