29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

Rooney amtabiria makubwa zaidi Ronaldo

134881LONDON, England

MSHAMBULIAJI wa timu ya Manchester United, Wayne Rooney, amekunwa na mafanikio aliyonayo Cristiano Ronaldo na akasema kuwa anavyoamini kuna mambo mazuri atayafanya staa huyo wa timu ya Real Madrid.

Hivi karibuni Ronaldo alifikia rekodi ya  Raul ya kuwa mfungaji bora wa muda wote  katika timu hiyo ya Real Madrid, ikiwa ni baada ya kuwa mchezaji tegemeo muda wote katika timu ya Taifa ya Ureno.

Rooney aliwahi kucheza  na Ronaldo akiwa Man United  kati ya mwaka  2003 na  2009 na anasema kuwa staa mwenzake huyo ataongeza rekodi ya upachikaji mabao.

“Nadhani ni mafanikio mazuri. Nimeshatuma ujumbe katika mtandao wa kijamii kumpongeza,” Rooney aliiambia tovuti ya Man United.

“Inashangaza sana ukiangalia mabao aliyoyafunga kila mechi,” aliongeza nyota huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles