25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Cheka ajiandaa kumtwanga Mashali

FRANCISI-CHEKA-PIX-NO-011NA ZAINAB IDDY, DAR ES SALAAM

BONDIA wa ngumi za kulipwa Tanzania, Francis Cheka, ameingia mafichoni kujiandaa na pambano lisilo la kuwania ubingwa la raundi 12  dhidi ya Thomas Mashali lililopangwa kufanyika Desemba 25, mwaka huu katika Uwanja wa  Jamhuri, mjini Morogoro.

Akizungumza na gazeti hili jana, Cheka alisema  kwa kuwa Mashali ameanza kumtangazia vita hadharani ameamua kuanza maandalizi mapema ili aweze kumpiga katika raundi za mwanzo.

Cheka alisema amepania kuweka historia mpya  kwa kumtwanga mapema mpinzani wake na kukata ngebe zake, huku akieleza kuwa kitendo chake cha kutamba kimemuongezea hasira,   hivyo atamstaafisha  kupigana ngumi mara baada ya kumwadhibu katika raundi ya tatu pekee.

“Yeye si anataka kuachana na masumbwi kwa kuweka historia ya kunipiga, basi ninaingia mafichoni kwa ajili yake na tutakapokutana ajiandae kupata kipigo cha historia kutoka kwangu,” alisema Cheka.

Cheka alisema ataonyesha vitendo kwenye ulingo ili aweze kuongeza heshima yake katika medani ya ngumi nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles