24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

KUTANA NA FAMILIA ‘ISIYOZEEKA’

FAMILIA ya Kichina imebamba katika mitandao ya jamii baada ya kuonekana haina dalili za kuzeeka kwa mujibu wa picha zao.

Msichana mmoja anayetumia jina la sysev7n  mtandaoni, alikuwa akisafisha picha za baba yake katika nyumba yao huko Chengdu.

Akiwa katika harakati hizo za usafi aliona kitu cha kushangaza katika picha hizo zile za zamani na za sasa.

Alilinganisha na picha zilizochukuliwa hivi karibuni na zile za zamani wakati wa utoto wake, akabaini kwamba wazazi wake wana mwonekano ule ule, yaani hawajazeeka.

Kufuatia ugunduzi wake huo, akazirusha katika akaunti yake kwenye mtandao wa jamii wa Kichina ujulikanao kama Weibo.

Picha hizo hazikuchukua muda kuwa gumzo kwa watumiaji wa mtandao kwamba familia hiyo imejaaliwa utajiri wa ujana, kwa mujibu wa mtandao wa People's Daily Online.

Mama na baba wote wana umri wa miaka 47. Picha ya baba wa mwanamke huyo, akiwa amepozi naye alipokuwa mdogo, ambayo ilipigwa miaka 18 iliyopita, ilionesha baba yake hajazeeka hata kidogo na yuko katika mwonekano alio nao sasa.

Picha zao za mtoko wao wa hivi karibuni mjini Chengdu pia ilionesha wazazi hao wenye utajiri wa ujana wakiwa pamoja na binti yao huyo.

Wazazi wake walionekana vijana mno kiasi kwamba baba yake watu walimdhania ni rafiki yake wa kiume huku mama yake wakidhani kuwa ni dada yake. 

Hali kadhalika bibi yake, ambaye ana umri wa miaka 67, ambaye pia alikuwa katika picha hiyo ya familia alionekana kana kwamba ni mama yake shukrani zikiendelea mwonekano wake wa ujana.

Maelfu ya watu walichangia kuhusu mwonekano huo wa ujana katika mitandao ya jamii ya China.

Wakati wengi wakiipongeza familia hiyo kwa mbaraka ya ujana waliyobarikiwa wana familia hao, wengine walihoji iwapo hakuna kisu kilichopitishwa katika ngozi yao ili waonekane vijana na au iwapo picha hizo hizo ni za kuchakachua.

Kufuatia uwapo wa baadhi ya maon hasi, ambayo alihisi yasingeipendeza familia yake, Sysev7n aliamua kuifuta post hiyo akisema hakutarajia kama watu wengi wanachangia picha hizo kiasi hicho. 

Aliongeza: “familia yangu haijawahi kufanyiwa upasuaji wowote wenye lengo la kuleta mwonekano wa ujana. Nilifuta post na ninatarajia watu hawataleta tena minong’ono yoyote yenye lengo baya nataka familia yetu iishi kwa amani bila songombingo za mitandaoni.'

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles