24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

Kupiga picha na Rambo Mil.2

LONDON, ENGLAND

Mashabiki ambao watakuwa tayari kupiga picha na staa wa filamu nchini Marekani, Sylvester Stallone, maarufu kwa jina la Rambo, atatakiwa kulipa zaidi ya milioni 2.

Msanii huyo atakuwa jijini London, Manchester na Birmingham kwenye tamasha la mitindo (UK events), ambalo litafanyika Agosti na Septemba mwaka huu, hivyo mashabiki ambao wanataka kupiga naye picha lazima walipe pauni 849, ambazo ni sawa na 2,481,880 za Kitanzania.

Mbali na kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kupiga picha na msanii huyo mwenye umri wa miaka 72, lakini tiketi za kiingilia kwa tamasha hilo zitakuwa zinauzwa pauni 125 hadi 325 sawa na 365,412 na 950,072 za Kitanzania.

Kikubwa ambacho kilionekana kuzungumziwa ni kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kupiga picha na staa huyo, baadhi ya mashabiki hawajapenda huku wengine wakidai inabidi wauze figo zao ili waweze kupata fedha kwa ajili ya kupiga naye picha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles