26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

Milioni 30 kushindaniwa Simiyu Jambo Festival

Derick Milton, Simiyu

Tamasha kubwa la michezo ambalo hufanyika kila mwaka katika mkoa wa Simiyu (Simiyu Jambo Festival) linatarajiwa kufanyika Juni 30, mwaka huu mjini Bariadi huku zaidi ya sh. Milioni 30 zikishindaniwa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 25, Mratibu wa tamasha hilo Zena Mchujuko amesema  maandalizi yamekamilika huku mgeni rasmi akitarajiwa kuwa Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzanaia, Dk. Tulia Ackson.

Amesema  jumla ya michezo minne itafanyika, ambapo kutakuwepo na mbio za baiskeli kwa wanaume na wanawake, mbio za riadha kilometa tano, baiskeli kwa walemavu.

“ Katika Tamasha hili ambalo wadhamini wakuu ni shirika la Idadi ya Watu Duniani (NFPA), likiwa limebeba kaulimbiu inayosema ‘Wezesha mtoto wa kike apate elimu atimize ndoto zake’ lengo lake ni kupiga vita mimba na ndoa za utotoni,” amesema.

Aidha amesema Sh. milioni 30 kushindaniwa kwa michezo yote, ambapo mshindi wa kwanza mbio za baiskeli kwa wanaume atapata 1, 000, 000,  Wanawake  700, 000, riadha 500, 000, na ngoma za asili mshindi atapata 1, 000, 000.

Kwa upande wake Mratibu wa UNFPA Mkoa wa Simiyu,  Dk.  Amir Batenga, amesema wao kama wadhamini waliona kutumia tamasha hilo katika kuokoa maisha ya wasichana ambao wamekuwa wakipata ujauzito katika umri mdogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles