28 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kuchauka: Siasa zimekwisha tuchape kazi

Na Asha Bani, Liwale

Mbunge wa Liwale, Zubeir Kuchauka amewataka wanaliwale kuacha kuendeleza siasa na badala yake kuchapa kazi.

Kuchauka amesema siasa Liwale zimekwisha na sasa nguvu zielekezwe katika kufanya kazi na kuijenga Liwale.

Hayo ameeleza jana wakati wa mkutano wa hadhara Liwale mjini viwanja vya Nanjinji uliokua na lengo la kuwashukuru wananchi na kusikiliza kero zao mbalimbali.

Mbali na kuwashukuru wananchi kwa kumchagua kwa kura nyingi lakini aliwataka kuacha siasa makundi na kuijenga liwale kwa umoja wao.

Kuchauka kipindi cha uchaguzi akiwemo yeye na diwani kuchomewa nyumba zao kwa moto,amesikitika kwa tukio hilo huku akiwataka sasa wananchi kufanya kazi.

Kuchauka ambaye ameunguziwa nyumba na gari tatu, na baadhi ya watuhumiwa tayari wanashikiliwa na jeshi la Polisi amesema wanaliwale ni wamoja na wanatakiwa kuwaza na kufanya mambo ya msingi baada yakuwaza vurugu ambazo hazina tija kwa mustakabali wa wanaliwale.

“Si mmeona nguvu hizo ambazo wananchi wanazifanya wanazichukua kuchoma nyumba gari la serikali ni kwa sababu hakuna nguvu zao walizowekeza na kusema tu mali ya serikali lakini kama wangechangia au wangechangia nguvu ya kujenga shule au hospital hakuna mtu angefanya uovu huo kwa kuhofia nguvu zake kupotea,”

“Basi tushirikiane kuanza sisi ujenzi wa shule hospitali ya wilaya halafu serikali inawekeza nayo nguvu zake humo tunasaidiana kujenga na sio kubomoa,” ameongeza Kuchauka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles