25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

KUBENEA ATOKA KIVINGINE, KUISHTAKI NEC BUNGENI


Na Bethsheba Wambura   |  

Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea, amekusudia kuwasilisha bungeni hoja binafsi ya kulitaka bunge kujadili mabadiliko ya katiba mpya itakayosaidia kupatikana kwa mfumo wa uteuzi wa Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ili utakaoruhusu tume hiyo kufanya kazi zake bila kufungamana na chama chochote cha siasa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Jumapili Machi 11, Kubenea amesema NEC ya sasa haiko huru na haina mamlaka ya kutosha kutokana na wafanyakazi na wajumbe wake wote akiwamo Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa tume hiyo kuteuliwa na Rais ambaye ni mwenyekiti anayetokana na chama cha siasa kitaifa hivyo kusababisha kuwepo na chembechembe za upendeleo katika uchaguzi.

“Nalitaka bunge liishauri serikali ilete bungeni muswada wa kubadilishwa kwa katiba mpya ili kuruhusu kuundwa kwa Tume huru ya uchaguzi ili kuweka wazi muundo juu ya kazi, mamlaka na mipaka ya tume hiyo katika kusimamia ma kuhakikisha kunakuwepo na chaguzi za huru na haki kwani muundo wa sasa haufai na haukidhi haja.

“Uchaguzi wa huru na haki hauwezi kufanyika kama hakuna chombo huru cha kusimamia uchaguzi huo, NEC ya sasa ni janga kwa taifa katika usimamizi wa uchaguzi jambo ambalo ni kinyume na katiba.

“Msimamizi wa uchaguzi hatakiwi kwa namna yoyote kujihusisha na chama chochote cha siasa isipokuwa tu ana haki ya kupiga kura kumchagua kiongozi amtakaye kama ilivyoruhusiwa katika katiba bila kuathiri utendaji kazi wake jambo ambalo litasaidia kupunguza vurugu zinazotokea baada ya uchaguzi moja ya sababau ikitajwa kutokuwa na imani na Tume ya uchaguzi,” amesema Kubenea.

Aidha Kubenea amependekeza kuanzishwa kwa mfuko wa fedha wa kujitegemea wa tume ili kuepuka kuomba fedha kwa serikali kila uchaguzi unapotaka kufanyika ili kuepuka kuchelewa kwa vifaa au siku za kufanyika kwa uchaguzi endapo wakichelewa kupata fedha kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles