26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kova humwambii kitu kwa Koffi

olomide1NA FARAJA MASINDE

KAMANDA mstaafu wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, amesema anachanganywa sana na wimbo wa Selfie wa Koffi Olomide kuliko nyimbo nyingine za nje.

Kova alitoa chaguo lake hilo alipokuwa akifanya mahojiano na kituo kimoja cha redio, ambapo alisema hata yeye kuna wakati ambao huwa anatumia kufuatilia muziki wa ndani na nje ya nchi.

Amedai kwamba katika kufuatilia nyimbo za nje ya nchi, ameguswa sana na wimbo wa Selfie ambao kila akiusikiliza lazima atingishe kichwa.

“Napenda kufuatilia muziki mbali na majukumu yangu ya kazi, nasikiliza muziki wa aina zote wa ndani na hata ule wa nje, nawasikiliza wasanii wote ninapokuwa na nafasi lakini kwa sasa wimbo ninaoupenda zaidi ni ule wa Selfie wa Koffie, kwa kuwa ni wimbo mzuri na kizuri lazima kipewe sifa zake,” alisema Kova.

Kova ni kati ya viongozi wachache ambao wanapenda tasnia ya muziki na wamekuwa wakitumia muda wao wa ziada kufuatilia sanaa hiyo, wakiungana na Rais mstaafu Jakaya Kikwete ambaye pia amekuwa karibu na sanaa ya muziki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles