27.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Wasanii nyota waongoza kukwepa mashirikisho ya sanaa

Godfrey MungerezaNA MWANDISHI WETU

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata), limeweka wazi kwamba wasanii wenye majina makubwa ndio wanaongoza kutokuwa wanachama wa mashirikisho ya wasanii.

Balaza hilo pia limeyataka mashirikisho na vyama vyote vya wasanii nchini kufanya uchaguzi ili kusaidia sekta ya sanaa iwe na mfumo bora wa utawala unaotambulika na kuheshimika na wadau, wasanii na Serikali kwa ujumla.

Katibu mtendaji wa baraza hilo, Godfrey Mungereza, alieleza hayo jana alipokuwa katika mkutano wa majadiliano kati ya Baraza na wadau wa sanaa nchini.

Baraza hilo pia limewataka wasanii wote nchini wajisajili ili wawe na vibali vya kazi za sanaa vitakavyowawezesha kushiriki kikamilifu kujenga mfumo wa utawala katika sanaa ambao utatumika kama mfumo sahihi na rasmi wa mawasiliano kati ya Serikali na wasanii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles