28.4 C
Dar es Salaam
Friday, February 23, 2024

Contact us: [email protected]

‘Korosho za Mtatiro’ zakamata 11 Tunduru

Mwandishi Wetu, Tunduru

Jeshi la Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wilayani Tunduru inawashililia makarani na waandishi 11 wa vyama vya msingi kwa tuhuma za kununua korosho za wakulima kwa fedha taslimu katika vituo vya kukusanyia korosho.

Makarani na waandishi hao wanatuhumiwa kujihusisha na ununuzi wa korosho kwa fedha taslimu katika vituo vya kukusanyia korosho na kisha kuziingiza kwenye mfumo rasmi wa stakabadhi ghalani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tunduru, Julius Mtatiro kuendesha operesheni maalumu ya kupambana na biashara haramu ya korosho maarufu jina la kangomba.

“Mmekuwa mkiwashinikiza wakulima wawaaachie korosho zao kisha mnawalipa fedha taslimu Sh 1,500 kwa kilo moja, na kisha korosho hizo mmekuwa mkiziingiza kwenye mfumo rasmi kwa kutumia majina ya matajiri waliowakabidhi fedha ili kufanya uhuni huo.

“Siyo tu kwamba mmeripotiwa na wakulima, bali hata korosho za mtego za DC zilipowafikia mlizinunua na ndipo tukabaini kuwa ninyi ni vinara wa kuvunja viapo vyenu vya kazi kwenye vyama vya msingi” amesema Mtatiro.

Pamoja na kukamatwa kwa watumishi hao 11 wa vyama vya Msingi wilayani Tunduru, Mtatiro amewasimamishakufanya majukumu yao na kuwapiga marufuku kujihusisha na masuala ya korosho kwenye vyama vya msingi katika msimu huu.

Pamoja na mambo mengine, pia Mtatiro amewataka viongozi wa vyama vya msingi ambavyo watuhumiwa hao wanafanya kazi, viwaondoe kazini mara moja ifikapo kesho Jumatatu.

“Nawahakikishia kuwa, ikiwa mtaendelea kujihusisha na mchezo huu wa hovyo, sitasita kuchukua hatua zile zile, kuwakamata, kuwaondoa kwenye shughuli za Amcos na kuwashtaki, korosho za DC zitawamaliza,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles