27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Koffi kutikisa Bongo na Royal Tour Septemba 10

Na Jeremia Ernest, Mtanzania Digital

MFALUME wa Rumba duniani Koffi Olomide ana tarajiwa kutua nchini katika onyesho maalum la kuunga mkono utalii wetu wa ndani kupitia filamu ya Tanzania Royal Tour, litakalo fanyika Septemba 10, katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Onesho hiloambalo ni mahususi kwa kutangaza utalii wa ndani limeandaliwa ungozi wa Jamhuri ya watu wa Kongo wanaoishi Tanzania, ambapo litakutanisha kampuni, tasisi, wafanyabiashara na wadau mbalimbali wa utalii na muziki hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam mapema leo Septemba 8, 2022 Rais wa watu wa Kongo, Lengosi VIP, amesema shoo hiyo itakuwa ya tofauti na maonyesho mengine ambayo Koffi amewahi kufanya hapa nchini.

“Tunaunga mkono juhudi za Rais wetu Samia Suluhu Hassan katika kitangaza utalii wa Tanzania ndiyo sababu tumeandaa onyesho hili ambalo Koffi amejipanga na kujizatiti kushusha burudani kali ya utalii ambayo hajawahi kuifanya hapa nchini na nje ya nchi,” amesema Lengosi VIP.

Naye mkali wa muziki wa Dansi hapa nchini, Nyoshi El Saadat amesema atakuwepo katika onyesho hilo akiwa na kundi lake la FM Academia tayari wamesha anza mazoezi kabambe kwa ajili ya kufanikisha siku hiyo.

Mbali ya wasanii wa dansi pia wata kuwepo Wanne Star na Mrisho Mpoto, ambao nao wata tumbwiza. Katika tamasha hilo kiingilio VVIP ni Sh milioni 10 VIP Sh milioni 5 na kawaida Sh 100,000.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles