27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Serikali yashauriwa kuanza na mapendekezo ya wadau wa habari bungeni

Na Mwandishi W etu, Mtanzania Digital

Serikali imeshauriwa kupeleka mapendekezo ya wadau wa habari katika bunge la mwezi huu (Septemba) kama ilivyoelezwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye.

Wito huo nunakuja kufuatia kuwapo kwa maandalizi ya serikali kutaka kuwasilisha Muswada wa Sheria ya Kulinda Taarifa Binafsi za Kimtandao.

Hayo yamebainishwa Septemba 8, mwaka huu na James Marenga, Wakili wa Kujitegemea ikiwa ni siku moja baada ya Waziri Nape kusema kwamba, ‘sheria’ hiyo imepata kibali hivyo Baraza la Mawaziri linatarajia kuwasilisha bungeni muswada wa sheria hiyo.

Wakati akifungua kongamano la siku mbili lililowakutanisha wadau mbalimbali wa Teknolojia ya habari na mawasiliano kutoka nchi mbalimbali barani Afrika Septemba 7, 2022, Waziri Nape alisema muswada huo wa sheria unatarajiwa kuwasilishwa bungeni Septemba 13, mwaka huu.

Wakili Marenga amesema, wadau wadau wa habari, wangependa kuona Waziri Nape anatimiza ahadi yake ya kuwasilisha mapendekezo ya wadau kuhusu mabadiliko ya sheria za habari katika bunge la mwezi huu.

“Wadau wangependa kuoana ahadi ya Mh. Waziri Nape ya kupeleka Mabadiliko ya Sheria ya Huduma za Habari yanafanikiwa kwenye Bunge hili la mwezi Septemba mwaka huu ili mchakato wa mabadiliko hayo ukamilike,” amesema Wakili Marenga.

Amesema, mjadala wa serikali na wadau wa Habari ulihusu Sheria ya Huduma za Habari 2016 na kwamba, kuna baadhi ya vipengele tayari wamekubakliana.

“Mjadala wa serikali na wadau ulihusu Sheria ya Huduma za Habari 2016, na yaliyojadiliwa ni mapendekezo ya wadau na yale ya serikali, kuna vipengele tulikubalia na vingine bado vipo kwenye mjadala,” amesema Marenga.

Akizungumzia sheria ya kulinda taarifa binafsi za kimtandao Wakili Marenga amesema, sheria hiyo si ya wadau wa habari pekee, inahusu watu wote.

“Halafu hii sheria ya data protection (ulinzi wa taarifa binafsi ) sio kwa ajili ya wadau wa habari pekee, ni sheria muhimu kwa watu wote,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles