23.4 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

KODI KWA WENYE NYUMBA SASA KUDHIBITIWA

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM


WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi amewatangazia kiama wamiliki wa nyumba wanaopangisha na kudai kodi ya mwaka mzima.

Akizungumza Dar es Salaam jana wakati wa uzinduzi wa jengo la makao makuu ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na sanamu ya Mwalimu Julius Nyerere, alisema kodi ya nyumba inatakiwa kutozwa kila mwezi badala ya mwaka mzima kama wanavyofanya baadhi ya wenye nyumba nchini.

“Mpangaji anatakiwa kulipa kodi kila mwezi labda atake mwenyewe kulipa kwa miezi zaidi ya mmoja. NHC hutoza kodi wateja wake (wapangaji) kila mwezi.

“Acheni tamaa, wenye nyumba chukueni kodi kila mwezi kwani huo ndio utaratibu,” alisema Lukuvi.

Aidha Lukuvi alisema kwa sasa Serikali ipo mbioni kuandaa muswada wa kuwabana wenye nyumba.

Alisema kwa sasa kuna vijana wanaoajiriwa wanashindwa kukaa jirani na mjini kutokana na kutozwa kodi ya nyumba kwa mwaka.

Kauli hiyo ya Lukuvi imetanguliwa na ile ya awali iliyotolewa bungeni Novemba 17, mwaka huu na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula, wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Halima Bulembo (CCM).

Katika swali lake, Halima alisema vijana ambao ni kati ya asilimia 56 na 60 nchini, wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na gharama kubwa ya kodi ambayo hutakiwa kulipa kwa kipindi cha mwaka mmoja au miezi sita.

Kutokana na swali hilo, Mabula alisema Serikali imeliona tatizo hilo na ipo katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa sheria ambayo itasimamia sekta ya nyumba, hivyo kuondoa changamoto ya wamiliki kudai kodi ya pango ya zaidi ya mwezi mmoja.

Alisema baada ya kukamilika kwa sheria ambayo itaunda chombo cha kusimamia sekta hiyo, wapangaji hawatalipa kodi ya mwaka wala miezi sita tena, bali watalipa kwa mwezi na kuweka amana ya miezi mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles