22.9 C
Dar es Salaam
Sunday, June 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kocha Al Ahly apata akili

ARP3649722NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

MATOKEO ya sare ya bao 1-1 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Al Ahly yameonekana kumfungua akili Kocha wa Al Ahly, Martin Jol, ambaye sasa anahaha kukipanga upya kikosi chake kwa ajili ya mchezo wa marudiano.

Martin Jol alieleza wazi kuwa Yanga ina kikosi kizuri chenye nidhamu ya mchezo, hivyo inawapasa kujipanga na kusaka ushindi nyumbani kwao.

Akizungumza baada ya mchezo wao dhidi ya Yanga, Jol aliweka wazi kuwa wana wakati mgumu kusaka matokeo mazuri kwao, akieleza kuwa watafurahi hata wakipata ushindi wa bao 2-0 ili uweze kuwavusha katika hatua nyingine.

“Hatuna namna tunafikiria kupata ushindi japo mambo si kama tunavyofikiria, tulijipanga kutafuta ushindi wa ugenini lakini naona wachezaji wangu walitaka sare tu, hivyo tuna kibarua cha kushinda nyumbani,” alisema.

Jol alisema Al Ahly ni timu kubwa lakini hawataidharau Yanga kwani katika mchezo wa soka lolote linaweza kutokea na kushangaza watu.

“Tutacheza nao kwa tahadhari, hatujipi uhakika wa kushinda mchezo huo kwani Yanga nao wana mipango yao, hivyo tunatarajia mchezo mgumu,”  alisema.

Timu hizo zinatarajia kurudiana Aprili 20 nchini Misri, mchezo unaotarajiwa kuwa wa kukata na shoka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles