23.3 C
Dar es Salaam
Sunday, June 16, 2024

Contact us: [email protected]

KMC yatuma salamu CAF

Glory Mlay

TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Mbeya Kwanza, katika mchezo wa kirafiki, uliochezwa jana kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.

Mabao ya mchezo huo yalifungwa na James Msuva katika dakika ya 15 na 45, huku Salum Kabunda akipachika bao moja dakika ya 88.

KMC ipo katika maandalizi ya mchezo wa marudiano dhidi ya AS Kigali wa Kombe la Shirikisho Afrika, unaotarajiwa kuchezwa Agosti 23, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa baada ya ule wa awali walitoka suluhu.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Kocha Mkuu wa KMC, Jackson Mayanja baada ya kumalizika kwa mchezo huo, alisema wachezaji wake wamecheza kwa umakini wa hali ya juu wameshambulia na wameweza kutumia nafasi walizopata kufunga mabao hayo.

Alisema kuelekea mchezo wao dhidi ya AS Kigali, hana wasiwasi kuwa kikosi kwani kimeonesha matumaini makubwa ya kufanya vyema katika mchezo huo.

Alisema kila mchezaji amepewa jukumu lake uwanjani kuhakikisha anajituma ili timu iweze kupata matokeo mazuri na kusonga mbele katika hatua inayofuata.

“Wachezaji wanapambana na hiyo inamaanisha uwezo tunao, kufungwa ni sehemu ya matokeo, hivyo hakuna tatizo lolote ambalo linatukwaza, tupo vizuri na tunajipanga kwa mchezo huo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles