25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 21, 2023

Contact us: [email protected]

Madrid wampigia debe Gareth Bale

MADRID, HISPANIA

MASTAA wa timu ya Real Madrid, wamemtumia ujumbe mfupi wa maandishi kocha wao Zinedine Zidane wakimtaka ampe nafasi mshambuliaji wao Gareth Bale kwenye kikosi cha kwanza.

Hatua hiyo imekuja baada ya mchezaji huyo kuonesha kiwango cha hali ya juu kwenye mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Hispania mwishoni mwa wiki iliopita dhidi ya Celta Vigo ambapo Madrid ilifanikiwa kushinda mabao 3-1.

Mbali na kutofunga bao kwenye mchezo huo, lakini alikuwa kwenye kiwango kizuri huku akihusika katika sehemu kubwa ya ushindi huo. Kutokana na hali hiyo, wachezaji mbalimbali akiwemo Casemiro, Thibaut Courtois na wengine.

“Bale ametupatia ubingwa, alifunga bao katika fainali na tukatwaa ubingwa Ligi ya Mabingwa Ulaya, tumekuwa tukimuheshimu wote kutokana na mchango wake ndani ya timu, anatakiwa kupata nafasi ya kucheza kwa kuwa ana uwezo mkubwa pia ni mtu muhimu kwetu,” alisema Casemiro.

Kwa upande mwingine mlinda mlango wa timu hiyo, Courtois alisema, “Bale ni mchezaji muhimu sana kwetu amekuwa na mchango mkubwa katika kila michezo mikubwa, anapendwa na kila mtu, tuna furaha tukiwa na mchezaji huyo kikosini,” alisema kipa huyo.

Kabla ya kuanza kwa msimu huu, Bale alikuwa miongoni mwa wachezaji ambao hawatakiwi na Zidane kwenye kikosi chake, hivyo alimtaka aondoke.

Hata kwenye ziara za timu hiyo kwa ajili ya msimu mpya, hakuwa anapata nafasi ya kucheza michezo ya kirafiki kwa kuwa Zidane alidai mchezaji huyo hayupo kwenye mipango yake ya msimu mpya wa ligi.

Bale alipata nafasi ya kucheza kwenye mchezo huo wa ufunguzi wiki iliopita kutokana na mshambuliaji wao mpya Eden Hazard kuwa majeruhi. Hata hivyo baada ya mchezo huo Zidane aliweka wazi kuwa, mchezaji huyo ataendelea kuwa naye msimu huu na hakuna mpango wa kumuuza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles