30.2 C
Dar es Salaam
Sunday, March 26, 2023

Contact us: [email protected]

Katwila atambia kikosi chake

Theresia Gasper-Dar es salaam

KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila, amesema kikosi chake kipo vizuri katika kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Kikosi hicho kilianza maandalizi kwa kuweka kambi ya wiki mbili jijini Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kucheza mechi moja ya kirafiki na baada ya hapo walirejea kwao Morogoro.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Katwila alisema kwa maandalizi waliyofanya kikosi chake kimekuwa fiti na wapo tayari hata ligi ianze sasa hivi.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha nakisifu kikosi changu kwa kujituma na kuonesha kile ambacho nakihitaji na tumejiandaa na ushindani wa Ligi Kuu,” alisema.

Alisema kwa sasa wanaendelea na maandalizi ya mwisho kabla ya ligi haijaanza, lakini wameshamaliza programu ya mazoezi ambayo walipanga kufanya katika kipindi hiki cha maandalizi.

Katwila alisema watafungua dimba dhidi ya Lipuli, hivyo wamejipanga kuanza kwa ushindi na kuanza mahesabu yao vizuri ili wajiweke katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,195FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles