27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

KMC yatangaza kocha mpya, Simkoko, Kondo waondolewa

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

ALIYEKUWA Kocha Msaidizi wa Simba, Hitimana Thierry, amejiunga na timu ya KMC kwa mkataba wa mwaka mmoja, huku uongozi wa timu hiyo ukiwafungashia virago John Simkoko na Habib Kondo waliokuwa wakikinoa kikosi hicho.

Kocha huyo ambaye alijiuzulu Simba hivi karibuni, amesaini mkataba huo leo Januari 6, 2022, mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusaini mkataba huo, Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, amesema wanaamini kocha huyo ataibadilisha KMC na kuirudisha katika ushindani wa Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kuanza kwa kusuasua.

“Mimi kama Meya ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya KMC FC na watendaji wengine tumesema lazima tujitafakari na tusikiliza kile mashabiki wetu na wataalamu walichokuwa wakisema na kutushauri.

“Leo nina furaha kuja mbele yenu kutangaza kuwa tumepata mwalimu mpya ambaye tutamkabidhi kikosi cha KMC, si mwingine bali ni Hitimana Thierry,” amesema.

Ameeleza kuwa wana imani na kocha huyo hadi kufikia kumpitisha, kulingana na uzoefu na elimu ya ukocha aliyokuwa nayo.

“KMC ina kikosi kizuri lakini ilikuwa ina kosa mbinu, tunaamini kocha Hitimana kwa uzoefu wake ataibadilisha timu,”amesema Mnyonge.

Kwa upande wake, Hitimana amesema amefurahi kujiunga na kikosi hicho, licha ya kuwa na muda mchache lakini atajitahidi kuhakikisha anaitengeneza KMC.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles