Sharifa Mmasi,Mtanzania Digital
MICHUANO ya Klabu Bingwa ya judo ya Majeshi Afrika Mashariki, yanatarajiwa kufanyika Desemba 6-12 mwaka huu mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na Mtanzania Digital leo Oktoba 21, Katibu wa Chama cha Judo Tanzania (JATA), Innocent Malya, amesema tayari nchi zote zina taarifa kuelekea mashindano hayo ambazo ni Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia na Burundi.
Malya amebainisha kuwa hadi sasa hawajapata mdhamini hivyo, wanafungua milango kwa wadau kujitokeza kuwaunga mkono katika kufanikisha michuano hiyo.
“Baada ya kumalizika kwa mashindano ya Klabu Bingwa sasa tunajiandaa na mtanange wa Klabu Bingwa kwa Majeshi, nitoe wito kwa wadau kujitokeza kuwaunga mkono ili tufanikishe kumpata bingwa,” amesema.