28.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 19, 2024

Contact us: [email protected]

Madaktari Marekani wafanikiwa kumpandikiza mgonjwa figo ya nguruwe

New York, Marekani

Kwa mara ya kwanza, figo ya nguruwe imepandikizwa kwa binadamu katika hatua ambayo inaweza kusaidia kupunguza uhaba mkubwa wa viungo vya binadamu vya kupandikiza, Shirika la Habari la Reuters limeripoti.

Utaratibu uliofanywa katika Kituo cha afya ch NYU Langone mjini New York ulihusisha utumiaji wa nguruwe ambaye jeni zake zilibadilishwa ili kuendana nayabinadamu na cha kufurahisha ni kwamba haikukataliwa na kinga ya mwili wa binadamu.

Mpokeaji alikuwa mgonjwa ambaye ubongo ulikua umekufa na dalili za ugonjwa wa figo ambaye familia yake ilikubali afanyiwe jaribio hilo kabla ya kutolewa kwenye mashine ya kumsadia kuishi, watafiti waliiambia Reuters.

Kwa siku tatu figo hiyo mpya ilipandikizwa kwenye mishipa yake ya damu na kuwekwa nje ya mwili wake ili kuwawezesha watafiti kuifikia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles