22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Kivule mabingwa Wazazi Cup

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Timu ya Wazazi Kivule imeibuka mabingwa katika mashindano ya mpira wa miguu kwa kuifunga timu ya Kitunda kwa mabao 2 – 0 katika mchezo uliochezwa uwanja wa Misitu.

Mashindano hayo yameandaliwa na Jumuiya ya Wazazi ngazi ya mkoa ambapo timu zinashindana kuanzia ngazi ya kata, jimbo, wilaya na baadaye mkoa.

Wafuasi wa timu ya Wazazi ya Kivule wakishangilia baada ya timu yao kuibuka washindi katika mchezo uliochezwa uwanja wa Misitu Kivule, Dar es Salaam. Wapili kulia ni Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Kivule, Reuben Mduma.

Mabao ya Kivule yalipatikana katika kipindi cha kwanza na cha pili ambapo wakati wote walionekana kutawala mchezo huo.

Mwenyekiti wa Wazazi Kata ya Kivule, Reuben Mduma, amesema timu ya Kivule itaungana na timu nyingine zilizoshinda katika kanda mbalimbali za Jimbo la Ukonga kisha kuchuana kupata timu zitakazowakilisha ngazi ya jimbo.

“Wanachama wamehamasika, tunaibua vipaji mbalimbali, washindi wataunda timu za majimbo kisha wilaya na baadaye tutapata timu ya mkoa,” amesema Mduma.

Naye Katibu Mwenezi Kata ya Kivule, Hemed Pogwa, amesema mashindano hayo yanawaleta wanachama pamoja na kuongeza hamasa na umoja katika chama hicho.

Amesema pia kupitia mashindano hayo kazi ya kufikisha utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kwa wananchi inakuwa rahisi zaidi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles