Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe amekipongeza Kitengo cha Mawasiliano na Jamii cha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa ufanisi na uharaka katika kufikisha taarifa kwa Wananchi.
Gondwe ametoa pongezi hizo jana baada ya utembelea mradi wa maji Rufu uliko Temeke jijini Dar es Salaam.
“DAWASA mmekuwa mstari wa mbele katika kuupasha umma habari zinazohusu Mamlaka yenu, kwnai mnatoa taarifa kwa haraka na kwa ufanisi jambo ammbalo linapaswa kuigwa na taasisi nyingine,” amesema Gondwe.
Gondwe amezitaka Taasisi nyingine za Serikali kuiga utendaji kazi na kuwajibika kutoa taarifa kwa wakati ili wananchi waweze kupata taarifa sahihi kwa wakati sahihi na kutoka sehemu sahihi ili kujenga Jamii yenye uelewa sahihi.
“Hivyo niwapongeze na niwasihi muendelee na kasi hiyo ili kuweza kufikia malengo mliyojiwekea,” amesema Gondwe.