31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Benki Exim yatangaza kupata faida licha ya changamoto ya Covid-19

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Benki ya Exim (Group) imetangaza kupata faida ya jumla ya Sh bilioni 25.3 (kabla ya kodi) kwa mwaka 2020, ikilinganishwa na hasara ya kiasi cha Sh bilioni 8.4 iliyopata kwa mwaka uliopita, hatua inayoakisi ukuaji wa asilimia 402  wa mwaka hadi mwaka.

Mafanikio hayo yanayotajwa kuwa yametokana na ufanisi wa kiutendaji licha ya changamoto za kiuchumi kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa COVID-19 ulioathiri ukuaji wa uchumi katika baadhi ya sekta muhimu nchini mwaka jana.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Exim, Jaffari Matundu (katikati) akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akizungumza kuhusu kuhusu utendaji wa benki hiyo katika kipindi cha mwaka 2020. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Mikopo wa benki hiyo, Zainab Nungu, ,  (Kushoto) na Afisa Mkuu Idara ya Fedha, Shani Kinswaga.

Kwa mujibu wa taarifa  iliyotolewa na benki hiyo jijini Dar es Salaam leo Februari 4, 2021 kupitia kwa Afisa Mtendaji Mkuu wake, Jaffari Matundu imebainisha kuwa benki hiyo imetekeleza kwa ufanisi mkubwa mkakati wa kushirikiana na sekta zinazofanya vizuri sambamba na kuongeza umakini zaidi katika matumizi yake ili kuongeza tija zaidi katika utendaji.

“Katika kipindi hicho benki ilikuwa bega kwa bega na sekta zilizoathiriwa wakati wa janga hilo na kwa kweli tulishirikiana kikamilifu na wateja wetu kuhakikisha kwamba si tu tunawapatia fedha bali pia tunawajengea uwezo wa kuweza kufanya shughuli zao katika kipindi hicho kigumu,” amesema Matundu.

Kwa mujibu wa, Matundu, hadi kufikia Desemba 31, mwaka jana, benki hiyo ilikuwa imetoa msamaha wa zaidi ya Sh bilioni 290  kwa njia ya likizo ya malipo na upanuzi wa vipindi vya ulipaji wa mikopo ili kusaidia wateja wa benki hiyo ambao biashara zao ziliathirika zaidi na athari za kiuchumi za Covid-19.

“Tunayo furaha kuripoti matokeo mazuri kwa mwaka wa fedha 2020. Tumefanikiwa kurejesha asilimia 9.0 ya faida kwenye mfuko wa wanahisa ikilinganishwa na marejesho hasi ya asilimia 9.2 mnamo 2019” amesema Matundu katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Nchini Tanzania, benki hiyo ilirekodi mafanikio makubwa kwa kupata faida (kabla ya kodi) ya Sh bilioni 18.8 kutoka kwenye hasara ya Sh bilioni 14.5 (kabla ya kodi) ya mwaka uliopita.

“Mafanikio hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa  mali kufuatia usafishaji uliofanywa katika kipindi hicho cha mwaka uliopita hatua iiyosababisha kupungua kwa mikopo chechefu kutoka asilimia 22.3 ya mwaka 2019  hadi kufikia asilimia 7.4 kwaka 2020.

“Matawi yetu ya nchini Djibouti na Comoro pia yalirekodi faida ya Sh bilioni 4.9 na Sh bilioni 5.7 (kabla ya kodi)  licha ya athari ya COVID-19.

“Jumla ya mali zetu imebaki kuwa Sh trilioni 1.9, Amana za wateja zimeongezeka kwa asilimia 4.4 wakati wa robo ya mwaka na kufikia Sh trilioni 1.38. Shughuli zetu nchini Tanzania, Comoro na Uganda zote zimerekodi ukuaji wa ajabu katika amana za wateja wakati wa robo ya mwisho wa mwaka,” ameongeza Matundu.

Amesema mafanikio hayo kwa kiasi kikubwa yanachochewa na kauli mbiu ya benki hiyo “Exim Kazini Leo kwa ajili ya Kesho” ambayo imekuwa ikiisukuma benki hiyo kubuni huduma mpya zinazoendana na mahitaji ya wateja wake

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles