26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

Gondwe ataka mradi wa maji Jet-Buza ukamilike kwa wakati

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Godwin Gondwe, ameipongeza Mamlaka ya Majisafi na usafi wa mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kwa hatua iliyofikia katika utekelezaji wa Mradi wa Maji Jet -Buza na kusisitiza mradi ukamilishwe kwa wakati ili wananchi waanze kupata huduma ya maji safi.

Mradi wa Maji Jet Buza unasimamiwa na kujengwa na (DAWASA) ukiwa na thamani ya Sh bilion 3.7 ukihusisha kazi ya kulaza mabomba ya inchi 16 kwa urefu wa Km 7.5 na kulaza mabomba ya usambazaji kwa urefu wa Km 37 na unatarajiwa kukamilika kufikia Aprili, mwaka huu.

Gondwe amesema, ni muda mrefu sana wananchi wa maeneo hayo wana shauku ya kupata huduma ya maji safi kwani chini ya uongozi wa Rais Dk. John Magufuli, mradi huo mkubwa utakaohudumia wananchi zaidi ya 10,000 umeweza kutekelezwa hivyo hauna budi kukamilika kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles