24.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 15, 2024

Contact us: [email protected]

TACAIDS kufikia uwiano wa unyanyapaa 2023

Na Faraja Masinde, Dar es Salaam

Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) imepanga kufikia mwaka 2023 kuwe kumefikia uwiano wa watu wenye mtazamo chanya kuhusu watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI (WAVIU).

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Jumanne Issango, wakati akifungua mafunzo elekezi kwa Watafiti wasaidizi juu ya Utafiti wa Unyanyapaa na Ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU Tanzania Bara.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa #TACAIDS Jumanne Issango akifungua mafunzo ya ukusanyaji wa takwimu za unyanyapaa na ubaguzi kwa Watu wanaoishi na VVU (WAVIU) utakaofanyika mapema mwaka huu 2021 Tanzania bara.

Amesema bado kuna vikwazo ambavyo vimeendelea kurudisha Tanzania nyuma kwenye mapambano dhidi ya virusi vya ukimwi jambo alilosema linatokana na ukosefu wa elimu hivyo utafiti huo utaleta mwanga mpya na hali halisi.

“Katika mkakati wetu wa mwaka 2022/23 wa kudhibiti Ukimwi nchini, suala la unyanyapaa limepewa kipaumbele, hivyo tumepanga ikifika kipindi hicho tuwe tumefikia uwiano wa watu wenye mtazamo chanya kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

“Hivyo tunataka ifike asilimia 100 kwa watu wote kuwatazama watu Waviu kwa jicho chanya bila kuwanyanyapaa, watu wafahamu na waelimishwe kuhusu unyanyapaa kwa waviu.

“Pia uwiano wa WAVIU au watu wanaonyanyapaliwa kwa kuishi na virusi vya ukimwi kwenye maeneo mbalimbali iwe asilimia 0, na uwiano wa watumishi wa vituo vya kutoleahuduma za Afya wenye hofu ya kuambukizwa VVU wanapotoa matunzo au huduma kwa WAVIU iwe asilimia 0,” amesema Issango.

Mratibu wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa kwa ajili ya utafiti wa kutambua hali ya unyanyapaa na ubaguzi kwa Watu wanaoishi na VVU (WAVIU), Yahaya Mmbaga akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo Isango amesema mikakati hiyo itafanikiwa iwapo watapata taarifa sahihi kutokana na utafiti huo unaokwenda kufanywa kwa WAVIU katika maeneombalimbali nchini.  

Aidha, Isango ameongeza kuwa: “Kumekuwa na unyanyapa wa aina mbalibali dhidi ya WAVIU kwani watu wanaona hata kuchangia vyombo na mtu huyo kuwa wanaweza kuwaambukiza jambo ambalo siyo la kweli, hivyo umuhimu wa utafiti huu utakapofanyika tutajua hali ilivyo nchini.

“Pia tutajua mapambano dhidi ya ukimwi yanaendeleaje na tuko katika hali gani, na hiyo itatusaidia kutengeneza mkakati mzuri wa kupambana na nyanyapaa na ubaguzi, kwani hauwezi kusema kwamba unapambana na kitu ilihali haukijui kiundani, hivyo lazima tutengeneze mkakati mzuri wa kuhakikisha kuwa tunaondokana na unyanyapaa na ubaguzi,” amesea Issango.

Washiriki wa mafunzo ya ukusanyaji wa taarifa kwa ajili ya utafiti wa kutambua hali ya unyanyapaa na ubaguzi kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU) wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi katika mafunzo hayo, baada ya kumaliza ufunguzi leo jijini Dar es Salaam.

Upande wake, Pantaleon Shoki, ambaye ni Mkurugenzi wa Utafiti kutoka Baraza la Watu wanaoshi na virusi vya Ukimwi (NACOPHA) amesema mafunzo hayo ya siku tatu yanahusisha vijana kutoka Halmashauri 31 nchini zikijumhisha watafiti wasaidizi 51.

“Tunaamini hatua hii ni muhimu kwani utafiti huu katika suala la unyanyapaa utatupatia majibu mengi ya maswali tunayojiuliza kulingana na madodoso tuliyoyaandaa.

“Kisha baada ya hapo utafanyika uchambuzi wa majibu hayo ambayo yataisaidia serikali pamoja na sisi wenyewe kuweza kuchukua hatua,” amesema Shoki.

Naye mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Lulu Nziku, kutoka Kasulu mkoani Kigoma amesema kuwa kupitia uwezo watakaojengewe itawasaidia kufanya utafiti huo kutokana na kuwapo kwa vitendo vya unyanyapaa.

“Jamii isichukulie watu wanaoshi na virusi vya Ukimwi kama wasioweza kitu cgochote jambo ambalo siyo sahihi hata kidogo,” amesema Lulu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles