MKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kandrick Lamar, amemkosha rais wa nchi hiyo Barack Obama kutokana na wimbo wake wa ‘Pay It Forward’.
Awali rais huyo alidai kwamba anavutiwa na msanii huyo kutokana na wimbo wake wa ‘How Much a Dollar Cost’ ambao aliuachia mwaka jana, lakini kibao hicho kipya cha ‘Pay It Forward’ kimezidi kumchanganya rais huyo na kuamua kumuita msanii huyo Ikulu.
Obama alitumia muda wake kujadili na msanii huyo juu ya kutoa elimu kwa watoto wa mitaani kama ilivyo katika wimbo huo mpya wa msanii huyo ambao unaonekana kumgusa rais.
“Nimefurahi sana kukutana na rais, kikubwa alinipa pongezi kwa kazi zangu na amedai kwa sasa ameguswa sana na wimbo wangu wa ‘Pay It Forward’ ambao unazungumzia vijana ambao wanahangaika na maisha ya mitaani,” alisema Lamar.