24.4 C
Dar es Salaam
Wednesday, June 19, 2024

Contact us: [email protected]

Jaguar amshambulia CMB Prezzo

jaguar-picNAIROBI, KENYA

MSANII wa muziki nchini Kenya, Charles Njagua ‘Jaguar’ amemshambulia mkali wa mastari CMB Prezzo kwa kitendo cha utovu wa nidhamu alichokionesha mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye runinga ya taifa nchini humo ya KTN.

Katika kipindi cha ‘Friday Briefing’ ambacho msanii anayealikwa hupewa nafasi ya kusoma taarifa ya habari, lakini katika mahojiano na mtangazaji wa kipinid hicho, Betty Klalo, Prezzo alionekana kukosa nidhamu ambapo alianza kwa kumsifia mtangazaji huyo ambaye ni mke wa mtu, huku akidai kwamba ni mzuri na mume wake ana bahati ya kuwa na yeye.

Ghafla Prezzo alionekana akimkumbatia mrembo huyo na kumfanya akose kujiamini katika kipindi hicho ambacho kikionekana ‘Live’.

Kutokana na hali hiyo Jaguar aliamua kumshambulia msanii huyo kwa njia ya mtandao wa kijamii wa Instagram na kudai kwamba ‘Prezzo anatakiwa kupelekwa kwenye kituo maalumu cha kuwasaidia watu ambao wana matatizo ya akili’.

Mbali na Jaguar, wadau mbalimbali wamemshambulia msanii huyo kwa kitendo cha kukosa nidhamu huku akiwa anahojiwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles