MKALI wa muziki wa Bongo Fleva, Bakari Hassani ‘Beka Ibrozama’, amesema anajivunia kuonyesha uwezo wake wa uimbaji kupitia wimbo wa Hello ulioimbwa na msanii Adele Adkins wa Uingereza.
Akiuzungumzia wimbo huo, Beka Ibrozama alisema kuwa hakuwahi kuimba kwa lugha ya Kiingereza kwa kuwa kuongea na kuimba ni vitu viwili tofauti, lakini alijitahidi kujifunza ili kufanya kitu chenye utofauti na kuonyesha kipaji chake.
“Wimbo umepata mapokezi makubwa tofauti na nilivyodhani, niwaombe mashabiki zangu wazidi kuniunga mkono kwani kazi ndiyo kwanza imeanza, wanaweza kuitazama Cover yangu ya Hello kwenye akaunti yangu ya Instagram au You Tube,” alisema Beka.
Beka alijizolea umaarufu mwaka 2011 mara baada ya kutoka na wimbo wa ‘Natumaini remix’ ambao alichanganya mashahiri ya nyimbo tofauti tofauti za wasanii wa Bongo Fleva.