25.5 C
Dar es Salaam
Wednesday, January 8, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Kipindupindu chaua wawili Dodoma

ganjaWATU wawili wamefariki dunia na wengine zaidi ya 120 wamelazwa katika vituo vya kutolea huduma ya kwanza katika wilaya tano za Mkoa wa Dodoma kutokana na ugonjwa wa kipindupindu.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Ofisa Afya wa Mkoa wa Dodoma, Edward Ganja alisema watu wawili wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo katika Wilaya ya Kongwa.

Ugonjwa wa kipindupindu umeripotiwa kuingia mkoani hapa tangu Septemba mwaka huu katika wilaya za Kongwa, Chamwino, Bahi, Manispaa ya Dodoma na Chemba.

Ganja alisema wagonjwa 120 walilazwa na kutibiwa katika wilaya hizo, ingawa sasa amebaki mmoja ambaye amelazwa hospitali ya mkoa.

Alisema kuwa Wilaya ya Bahi ilikuwa na  wagonjwa 78 ambao wametibiwa na kupona, Chamwino 12, Chemba wawili na Kongwa 35 mbali na wawili waliofariki dunia.

Pamoja na hali hiyo, Ganja alisema uongozi wa mkoa umechukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa wananchi.

“Pia tumekuwa tukitoa elimu kupitia Serikali za vijiji na kamati za afya kwa kufanya ukaguzi nyumba hadi nyumba.

“Kamati hizo zina mamlaka ya kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula shuleni na pombe za kienyeji ambazo ni chanzo cha kupata vijidudu vya ugonjwa huo,” alisema Ganja.

Aliwataka wakazi wa Dodoma kuhakikisha wananawa mikono kabla na baada ya kula, kula vyakula vya moto na kuzingatia kanuni za usafi ili kuepuka ugonjwa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles