29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa mbio za Mwenge aweka jiwe la msingi mradi wa maji wa Bilioni 17 Mlandizi, Msoga

Na Mwandishi Wetu, Pwani

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi, amezindua mradi wa maji wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wenye thamani ya Sh biloni 17.3 eneo la Msoga Chalinze mkoani Pwani.

Akizungumza baaada ya kuwasili eneo hilo alitembelea mradi huo na kukagua ujenzi wa matenki na mifumo ya mabomba ya kuunganishia maji ambapo ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.

“Nimefurahishwa na hatua mliofikika katika ujenzi wa mradi huu nakata mwakikishe mradi huo unaisha kwa wakati ili wananchi waweze kupata maji kama Rais Samia Suluhu Hassan alivyoagiza kutaka kero ya maji kwa wananchi inapungua au kuisha kabisa,” amesema Luteni Mwambashi.  

Awali kabla ya kukagua mradi alipokea taarifa fupi ya mradi huo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Mhandisi Cyprian Luhemeja ambaye alielezea mradi huo wenye thamani ya zaidi  ya Sh bilioni 17 ambao umekamili kwa asilimia 95 kutandaza mabomba zaidi ya kilometa 50 na kukamilisha ujenzi wa matenki makubwa ya kupokelea maji kutoka kwenye chanzo, ambapo alisema mradi utatanufanisha wananchi wa  vijiji vya Kara, Mbara, Pingo na Chalinze na unatarajia kuzinduliwa mwezi wa 9 mwaka huu.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Luteni Josephine Mwambashi, akizindua jiwe la msingi la mradi wa maji wa Mlandizi-Mboga uliyopo wilayani Chalinze mkoani Pwani leo.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles