23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

COSOTA yaahidi kuzingatia maoni ulipaji mirabaha

Na Anitha Jonas, Mbeya

Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) ya ahidi kuzingatia maoni ya yaliyotolewa na Wamiliki wa Vyombo vya Habari Nyanda za Juu Kusini katika Kanuni mpya za Leseni ya Utangazaji na Maonesho kwa umma.

Kauli hiyo imetolewa leo jijini Mbeya na Mwanasheria wa COSOTA,  Lupakisyo Mwambinga  baada ya kueleza lengo la  kuundwa kwa kanuni hizo na kuwapitisha wadau hao.

“Pamoja na kwamba mtakuwa mnatoa maoni kwa kuzungumza naomba pia mjaze fomu ya maoni ili tuweze kupata maoni yenu kwa njia ya maandishi kila mmoja ajaze fomu hiyo ,tutahakikisha tunazingatia maoni yote mtakayotoa,”amesema  Mwambinga.

Akizungumza katika kikao hicho cha wadau  Mwambinga  amesema sheria ya Hakimiliki nchini inaeleza wajibu wa watumiaji wa kazi za muziki  na kulipa mirabaha hivyo suala la ulipaji wa tozo hiyo. Kwa upande wa Meneja wa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Mhandisi Alinanuswe John, amewapongeza wamiliki wa vyombo vya habari  kwa kushiriki kikao hicho na kuwasihi wazungumze kwa hoja na waache kuwa na hasira wanapochangia hoja  kwa sababu kikao hicho kimelenga kuweka mazingira rafiki ya ulipaji wa tozo hiyo ya mirabaha

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles