23.7 C
Dar es Salaam
Saturday, September 23, 2023

Contact us: [email protected]

BetWay yajipanga kuwapa raha mashabiki wa soka nchini

Na BEATRICE KAIZA, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya Kimataifa michezo ya kubashiri  ya BetWay, imezinduliwa Tanzania, huku ikijipanga  kuunga mkono jitihada za Serikali za kuendeleza  soka kuanzia ngazi za chini na  kuwapa  burudani mashabiki mchezo huo.

Hayo yamesemwa na Meneja Uendeshaji, Jimmy Masaoe  alipozungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa  kampuni hiyo   leo jijini Dar es Salaam.

Amesema    Betway ni kampuni ya kubashiri iliyosajiliwa Tanzania, huku ikiwa ni mdhamini  wa klabu ya West Ham United ya England.

“Ni wakati mzuri katika sekta ya michezo ya kubashiri na tunaamini kwa uzinduzi wa bidhaa hii yenye ubora wa kimataifa kwenye soko, tunauwezo wa kuleta msisimko kwa wanaobashiri na mashabiki, wakati bado tunarudisha kwa jamii kupitia miradi mbali mbali ya michezo.”

“Betway tumejipanga kuwekeza zaidi Tanzania kwa lengo la kukuza  na  kuendeleza mchezo wa soka na leo rasmi tumefanya uzinduzi, tunahakikisha tunazifikia hadi timu za madaraja ya chini,” amesema Masaoe.

Kwa upande wa Meneja Masoko wa  kampuni hiyo  nchini Tanzania, Calvin Mhina, amesema kuwa kuisapoti michezo katika jamanii ni kitu cha muhimu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,699FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles