28.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi mbio za Mwenge agoma kuzindua mradi wa maji Kilimanjaro

Safina sarwatt – Mwanga

Kiongozi wa Mbio za mwenge wa uhuru kitaifa, Mzee Mkongea Ally, amekataa kuzindua mradi wa maji  Katika  kata ya Kwakoa wilayani Mwanga Mkoani Kilimanjaro, uliogharimu zaidi shilingi milioni 205, kutokana na kuwepo kwa ubadhilifu mkubwa wa fedha katika ujenzi wa mradi huo na kuagiza waliohusika watafutwe popote walipo ili wachukuliwe hatua za kisheria.

Mzee Mkongea amesema kuwa baada ya kukagua mradi huo wamebaini kwamba  kuna ubadhilifu wa fedha katika ujenzi wa mradi huo kwani hauendani na fedha zilizotolewa na serikali na kwamba wametilia shaka utaratibu uliotumika katika ujenzi wa mradi huo kutokana na kwamba taarifa zinaonyesha kuna kandarasi lakini kuna taarifa inasema fedha zilitoka kwenye mfuko halmashauri.

Amesema kuwa kuna watu waeindanganya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na kutumia fedha za umma za kinyume na taratibu na kwamba utaratibu wa ujenzi unaelekeza kwamba vipimo vya  vifaa vya ujenzi unafanyika kabla ya ujenzi lakini hapa inaonyesha ujenzi ulianza kabla.

“Tumeitilisha shaka ujenzi wa huu mradi kwasababu hiyo mwenge wa uhuru hauwezi kuzindua mradi huo wahusika wote watafutwe popote pale walipo wachukuliwe hatua za kisheria mara moja ,”alisema.

“Mkuu wa wilaya, Takukuru ninawapa wiki mbili  hakikisheni wahusika hao wote wamepatikana ili hatua za kisheria zichukuliwe Mwenge wa uhuru haumwonei mtu bali inatenda haki,”alisema.

Kwa upande wake Mhandisi wa Maji wilaya ya Mwanga Musa Njuki, amesema kuwa ujenzi wa mradi huo ulianza mwaka 2017 ambapo fedha za ujenzi huo zimetoka serikali kuu pamoja halmasahuri .

“fedha kutoka serikali kuu ni zaidi milion 205 na nyingine zimetoka kwenye mfuko wa halmashauri, binafsi nimehamia mwaka 2018 na nilikuta ujenzi ukiwa umekamilika,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles