26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Kotei awaaga mashabiki Simba, akumbuka walivyoitwa ‘wa matopeni’

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Aliyekuwa mchezaji wa Timu ya Simba SC ya Dar es Salaam, James Kotei (25) amewaaga mashabiki wa timu hiyo kwa staili ya aina yake akiwaandikia ujumbe mzito huku akikumbuka walivyoitwa ‘wa matopeni’.

Kotei aliyechezea Simba misimu miwili mfululizo tangu mwaka 2016, akitokea katika klabu ya Al-Oruba ya nchini Oman, amesajiliwa na Klabu ya Kaizer Chiefs ya nchini Afrika Kusini inayoshiriki ligi kuu nchini humo kwa mkataba wa miaka mitatu.

Raia huyo wa Ghana ameandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa Instagram leo Jumatano Juni 26, uliobeba hisia za huzuni na majonzi na shukrani kwa washabiki wa Simba.

“Kwa washabiki wangu wapendwa wa Simba, siku ya kwanza nilipokanyaga katika ardhi hii nzuri nilijihisi upendo, na siku ya kwanza nilipovaa jezi ya Simba nilijivunia kuwa mmoja kati ya klabu hii ambayo kuna mapenzi ya mpira kwa kila mtu.

“Siwezi danganya kila sekunde niliyokuwepo hapa ilikuwa nzuri kwa miaka miwili na nusu iliyopita ila nadhani muda wa kusema kwa heri umefika japo haukutarajiwa, siku zote nitakumbuka siku tuliposhinda kombe kule Dodoma na kujifungulia uwanja wa mpira kimataifa na tangu siku hiyo waliacha kutuita ‘Wamatopeni’.

“Nakumbuka Kombe letu la kwanza la ligi na la pili, lakini siku tulipofuzu kuingia katika robo fainali za michuano ya Klabu Bingwa Afrika zilikuwa kumbukumbu bora sana kwetu sisi sote, siwezi kumshukuru kila mmoja kwa jinsi mlivyofanya nijihisi upendo, hakika nawashukuru nyote kwa kuifanya Tanzania kuwa nchi yangu ya pili.

“Akili imechanganyikiwa hapa ninavyojiandaa kupambana na changamoto nyingine lakini kamwe sitoisahau Simba SC, mandhari nzuri ya jiji la Dar es Salaam na lugha ya Kiswahili ambayo nilishaanza kuijua inavyozungumzwa.

“Nawapenda sana ila samahani hakikisheni mnaisapoti Simba katika mvua na jua, natumai siku moja matarajio yetu yatafikiwa, asanteni kwa kila kitu na nawapenda sana,” ameandika Kotei.

Aidha, kupitia ukurasa wao wa Instagram Klabu ya Kaizer imethibitisha kumsajili Kotei kwa mkataba wa miaka mitatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles