20.9 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Navy Kenzo wapata mtoto wa pili wa kiume

Betsheba Wambura, Dar es Salaam

Wasanii wa muziki wanaounda kundi la Navy Kenzo, Aika Marealle maarufu Aika na Emmanuel Mkono maarufu Nahreel, wamejaaliwa kupata mtoto wa pili wa kiume waliyempa jina la Jamaica.

Wawili wao wameweka wameweka wazi kupitia kurasa zao za Instagram, Aika akitupia picha ya mwanamke ambaye ni ndugu yake akiwa amebeba mtoto huku Nahreel akitupia picha ya mtoto amelala.

Katika ujumbe huo Aika aliandika; “Jamaica is here God is good ( Jamaica yuko hapa), asanteni kwa maombi yenu.”

Hata hivyo, jina na jinsia la mtoto huyo lilishawekwa hadharani na Aika wiki chache zilizopita Wawili hao tayari wana mtoto wa kwanza wa kiume anayejulikana kwa jina la Gold aliyezaliwa Jumamosi ya Desemba 9, mwaka 2017.

Aika na Nahreel, wamekuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi kwa zaidi ya miaka 10 hadi sasa na wamekuwa wakishirikiana katika kazi zao za sanaa na wamewahi kushinda tuzo kadhaa za muziki ikiwamo ya Sound City zilizotolewa nchini Nigeria kama kundi bora.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles