29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongera akabidhiwa jezi ya Mosoti Simba

Mshambuliaji mpya wa Simba, Paul Kiongera
Mshambuliaji mpya wa Simba, Paul Kiongera

NA HUSSEIN OMAR, UNGUJA

MSHAMBULIAJI mpya wa Simba, Paul Kiongera, amewasili katika kambi ya timu hiyo, iliyopo mjini hapa kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayoanza Septemba 20, mwaka huu.

Simba imeweka kambi hapa ikiwa chini ya Kocha Mkuu wake, Mzambia Patrick Phiri na Jumamosi inatarajia kucheza mechi ya kirafiki na Gor Mahia ya Kenya, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Kiongera, aliyewasili hapa juzi usiku, jana alijumuika na wachezaji wenzake katika mazoezi ya ufukweni, akiwa amevalia jezi namba tano iliyokuwa ikitumiwa na beki Mkenya, Donald Mosoti.

Hatua ya Simba kumwondoa Mosoti kikosini, imekuja baada ya timu hiyo kumsajili mshambuliaji Mganda, Emmanuel Okwi, ili kuendelea kubaki na wachezaji watano wa kigeni kwa mujibu wa kanuni za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Wachezaji wengine wa kigeni waliopo katika kikosi cha Simba ni Mganda Joseph Owino na Warundi Amisi Tambwe na Pierre Kwizera.

Hata hivyo, Okwi ameingia katika mgogoro na klabu yake ya Yanga ambayo imesema inamtambua kama mchezaji wake akiwa na mkataba wa miaka miwili zaidi, baada ya kuwatumikia kwa miezi sita.

TFF ndiyo itakayokata mzizi wa fitina baada ya kukutana na pande hizo mbili mwishoni mwa wiki hii na kutoa uamuzi ambao ndio utakaotoa mwelekeo wa Mganda huyo kuichezea timu gani msimu ujao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles