28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Yanga kuivaa Thika United Taifa leo

Kikosi cha Yanga
Kikosi cha Yanga

NA JENNIFER ULLEMBO, DAR ES SALAAM

KIKOSI cha timu ya Yanga leo kinatarajia kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya Thika United ya Kenya katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga, iliyoweka kambi visiwani Zanzibar, ilirejea Dar es Salaam baada ya kucheza mechi tatu kujiandaa na Ligi Kuu Tanzania Bara, itakayoanza Septemba 20, mwaka huu.

Kabla ya kuanza kwa ligi hiyo, Yanga watamenyana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, timu ya Azam FC, katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa Septemba 13, katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.

Yanga ilishinda mechi zake zote ikiwa visiwani humo, ikianza kwa kuichapa Chipukizi bao 1-0, katika Uwanja wa Gombani, kisha kuifunga Shangani mabao 2-0 na kumaliza kwa kuwalaza mabingwa wa Ligi Kuu ya Zanzibar, timu ya KMKM, mabao 2-0 katika mechi zilizochezwa katika Uwanja wa Amaan.

Akizungumza jana, Ofisa Habari wa Yanga, Baraka Kiziguto, alisema Thika United wamewasili jijini jana tayari kwa mchezo huo.

“Mashabiki wajiandae kuiangalia timu yao ambayo kwa kipindi kirefu hawajaishuhudia ikicheza michezo ya kirafiki tangu ichukuliwe na Kocha Marcio Maximo,” alisema Kizuguto.

Katika mchezo huo, mashabiki na wanachama wa Yanga watapata nafasi ya kuwaona kwa mara ya kwanza wachezaji wawili raia wa Brazil, Andrey Coutinho na Geilson Santos ‘Jaja’.

Yanga inatarajia kuanza ligi kwa kucheza dhidi ya Mtibwa Sugar, katika Uwanja wa Jamhuri, mkoani Morogoro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles