28.7 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

King Sugerrr afungua mwaka na ‘Donnez Moi’

California, Marekani

Msanii wa miondoko ya Afro Genge kutoka California, Marekani, King Sugerrr, amefungua mwaka 2021 kwa kuachia video ya wimbo, Donnez Moi kutoka kwenye albamu yake fupi (EP) inayoitwa Hiboux.

Sugerrr amesema video ya wimbo huo ni miongoni mwa nyimbo sita zinazopatikana kwenye EP hiyo ambayo imetoka hivi karibuni na kupokewa kwa kishindo na mashabiki wa muziki huo katika mitandao kadhaa ya kusikiliza na kununua muziki duniani.

“Nimeanza vizuri mwaka 2021 kwa sababu EP yangu imewafikia mashabiki wengi na sasa nitakuwa naachia video moja moja kama ambavyo nimeanza kwenye wimbo wa Donnez Moi, video ipo YouTube naomba ushirikiano kwa mashabiki zangu wa Afrika Mashariki ili nizidi kuitangaza Afro Genge hapa Marekani,” amesema King Sugerrr.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles