27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Zabron Singers washinda Maranatha Awards Marekani

Na Christopeher Msekena, Dar es Salaam

Kundi maarufu la muziki wa Injili nchini, Zabron Singers, limeshinda kipengele cha kundi linalokuja kwa kasi Afrika (Most Promising Music Group Africa) kwenye tuzo za Maranatha zilizotolewa hivi karibuni huko Maryland, Marekani.

Huo ni mwendelezo wa Zabron Singers kutoka Kahama kushinda tuzo ambapo mwaka 2019, walishinda tuzo mbili nchini Kenya kupitia wimbo wao maarufu Tumeuona Mkono wa Bwana pia wakanyakua tuzo ya Chomoza Gospel Music hapa Tanzania.

Mwenyekiti wa kikundi hicho, Marco Joseph Bukuru, amesema wanashukuru wapenzi wa muziki wao wa ndani na nje ya nchi kwa kufanikisha ushindi wa tuzo hiyo waliyoipata kupitia wimbo, Nakutumia Wimbo ambao umetazamwa na watu zaidi ya milioni 4.4 kwenye chaneli yao ya YouTube.

“Tuzo zimetolewa Marekani kwahiyo sisi pamoja na washindi wengine wa hapa Tanzania tutazipokea hivi karibuni zitakapoletwa nchini. Tumeuanza mwaka 2021 tunaahidi kuwapa nyimbo zingine nzuri zenye kuponya kuokoa kufariji na kujenga ili sifa zimrudie Mungu,” amesema Bukuru.

Mwalimu wa Zabron Singers, Japhet Zabron ambaye wiki hii ameachia wimbo wake wa ‘Niombee’, amesema kwa nguvu ya Mungu na mashabiki wamefanikiwa kuzalisha nyimbo kama Tumeuona Mkono wa Bwana uliotazamwa na watu zaidi ya milioni 30, Sweetie Sweetie unaoendelea kufanya vizuri kwenye sehemu mbalimbali ikiwemo kwenye sherehe za harusi huku video yake ikiwa imetazamwa na watu milioni 3 ndani ya mwezi mmoja katika channeli yao ya YouTube.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles