26.7 C
Dar es Salaam
Saturday, February 24, 2024

Contact us: [email protected]

Watatu kortin kwa uhujumu uchimi Moshi

Safina Sarwatt , Moshi

Washtakiwa watatu wamefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi na kuunganishwa kwenye kesi ya uhujumi uchumi inayowakabili washtakiwa sita na kufikia idadi ya washitakiwa tisa na kusomewa mashtaka saba.

Washitakiwa hao watatu ni Tumaini Tesha, Charles Juma na Devis Mtui.

Akisoma mashitaka hayo na wakili wa serikali, Sabitina Mcharo mbele ya hakimu wa mahakama hiyo, Meku Massawe, amedai kuwa washitakiwa wanakabiliwa na makosa saba.

Wakili Mcharo amedai katika kosa la kwanza washitakiwa kwa pamoja na wenzao sita ambao hako mahakamani walifanya muungano wakufanya kosa katika eneo lisilofahamika, kosa lingine kuharibu mali ambayo inatoa huduma, wizi wa taa za solar panels 16 na betri za solar 16, mali ya anispaa ya Moshi,yenye thamani ya Sh milioni 59.4

Aidha, amedai kosa lingine linahusu umiliki wa mali visiyo halali inayomkabili mshtakiwa wa tatu, Germana Massawe ambaye hakuwepo mahakamani .

Wakili huyo amedai kwamba kosa lingineni kuharibu mali ambazo Mamlaka ya Manispaa ya Moshi nakusababisha hasara.

Washitakiwa wengine sita ni Donald Machange, Goodluck Shuma, German Massawe, Moses Kiresoi, George Kavishe na Alex Lomnyaki na kwamba washtakiwa hao waliiba sola na paneli katika maeneo mbalimbali kwa nyakati tofauti na kwenda kuziuza.

Wakili Mcharo amedai washtakiwa kwa pamoja watenda makosa hayo katika maeneo mbalimbali ya manispaa ya Moshi mkoni Kilimanjaro.

Aidha, hakimu Meku Massawe amesema washitakiwa hao hawaruhusiwi kujibu chochote na kwamba upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika wa kesi hiyo itatajwa tena Januari 25, na washtakiwa wamerudishwa mabusu ya Karanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles