King Joshua aachia video ‘Tupo Hapa’

0
526

Minnesota, Marekani

Mwimbaji wa nyimbo za Injili, King Joshua, kutoka Minnesota, Marekani ametambulisha video ya wimbo wake mpya unaofahamika kama Tuko Hapa uliobeba ujumbe mzuri wa kumsifu Mungu.

Kwa mujibu wa King Joshua, mtu yeyote anaweza kuusikiliza na kubarikiwa nao.

“Katika kila hali tunapaswa kuendelea kusifu na kumwabudu Mungu, video tayari nimeiachia na sasa ipo kwenye chaneli yangu ya YouTube na kila mtu anaweza kuitazama na kubarikiwa, naomba sapoti kwa mashabiki zangu hapo Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla,” amesema King Joshua.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here