29.4 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

Mbunge Mwanga amlilia Hayati Dk. Magufuli

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mbunge wa Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro, Joseph Tadayo ameelezea kusikitishwa kwake na kifo cha aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kilichotokea Machi 17, mwaka huu jijini Dar es Salaam kwa matatizo ya moyo na kutoa wito kwa wananchi na viongozi kumuenzi kwa mambo matatu.

Tadayo ameyataja mambo hayo matatu kuwa ni pamoja na kuwa kithubutu, uzalendo na kuona mbali kiongozi anayethubutu, mzalendo, na kuona mbali huku akisisitiza kuwa alikuwa ni kiongozi anayejiamini kwa kile ambacho anakifanya kwa taifa lake.

Tadayo aliasema hayo juzi Machi 19,2021 wakati akiongea na www.mtanzania.co.tz kwa njia ya simu akiwa jijini Dodoma na kuongeza kuwa kifo cha Rais Magufuli ni pigo kubwa kwa taifa na ameacha historia kubwa nchini na Kimataifa.

Amesema Rais Dk. Magufuli ni shujaa wa Afrika na kwamba viongozi waliochaguliwa na wananchi hawana budi kumuenzi kwa kutekeleza kwa vitendo uthubutu wa kufanya maamuzi na hivyo tutaweza kutekeleza miradi tuliyowahaidi wananchi.

Tadayo ambaye ana taaluma ya Sheria amesema Rais Dk. John Magufuli ni shujaa ni kiongozi ambaye anajiamini kwa kile ambacho anakifanya kwa maslahi ya taifa .

“Alikuwa kiongozi anayeona mbali na kufikiria makubwa kwa ajili ya ujenzi wa taifa ikiwemo miradi mikubwa ya maendeleo ya kitaifa,”amesema Tadayo ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Amesema vitu atakavyokumbukwa navyo Hayati Dk. Magufuli ni pamoja na kukuza uchumi wa taifa kutoka nchi masikini hadi kuifikisha Tanzania katika Uchumi wa Kati, ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Nyerere, ujenzi wa reli ya kisasa ya mwendo kasi na uboreshaji wa miundombinu ikiwamo barabra za juu (Fly Over).

Tadayo amesema Rais Magufuli atakumbukwa kwa kupigania haki za wananchi wanyonge na kupambana na wezi na mafisadi wa fedha na mali za umma na wahujumu uchumi wa taifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles