Christopher Msekena
MSANII mwenye umri mdogo kutoka Zimbabwe, Ngonidzashe Dondo a.k.a King 98, amesema staa wa muziki nchini Nigeria, Davido, alimchongea njia ya kukutana na Diamond Platnumz mpaka wakafanikiwa kufanya kolabo yao, Kachiri.
Akizungumza na MTANZANIA hivi karibuni jijini Dar es Salaam, King 98 ambaye yupo Tanzania kwa ziara ya kimuziki, alisema licha ya ukubwa wa Diamond ni mtu mnyenyekevu aliyempa ushirikiano mwanzo mpaka mwisho.
“Nilikuwa nafanya vizuri Afrika Kusini na wimbo, Wacko niliofanya na Nasty C pia nimeshafanya ngoma na Davido inayoitwa No Bad Vibes. Davido ndio alipendezkeza nifanye ngoma na Diamond, tukawasiliana tukapanga namna ya kukutana tukafanya audio na video ya Kachiri.
“Wakati tunafanya video ya Kachiri niligundua Diamond ni mtu ‘hambo’ sana, amenishika mkono na akaweka asilimia 100 ya nguvu zake kwenye kazi yangu, naweza kusema ilikuwa rahisi kufanya naye kazi,” alisema King 98.