27.7 C
Dar es Salaam
Saturday, June 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kim Kardashian amwachisha mwanaye kunyonya

Kim na SaintNEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, ameweka wazi kwamba amemuachisha mwanaye kunyonya Saint West kwa sababu ya mtoto wake wa kwanza North West kuwa na wivu.

Saint ambaye alizaliwa Desemba mwaka jana, ameachishwa kunyonya kutokana na dada yake North mwenye umri wa miaka miwili kuona wivu wakati mtoto huyu akiwa ananyonya.

Inadaiwa kwamba kila wakati Saint akiwa ananyonya basi North lazima alie huku akionesha wazi kwamba hapendi mtoto huyo anyonye.

“Nimeona bora nimuachishe Saint kunyonya, maana kila wakati akiwa ananyonya basi North lazima alie na aje kumtoa kwa nguvu.

“Hiyo inaonesha kwamba ni wivu, hivyo nimeona bora niwe namnunulia maziwa kuliko kumnyonyesha mbele yake, hata hivyo wiki hii North aliniambia kwamba wala hachukii kumuona mdogo wake akinyonya na hana mpango wa kulia tena,” alisema Kim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles