MTOTO wa mtayarishaji wa muziki nchini Marekani, Kasseem Dean ‘Swizz Beatz’ ambaye anajulikana kwa jina la Egypt Dean, amemtisha baba yake kwa kipaji alichokionesha cha kutengeneza midundo ya muziki.
Mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitano, amekuwa akiingia studio kila siku kumtazama baba yake wakati anapotengeneza midundo mbalimbali ya muziki wa hip hop na RnB.
Juzi baba yake alishikwa na butwaa baada ya mtoto huyo kumkuta akiwa katika mitambo hiyo na kuanza kutengeneza mdundo.
“Si kitu cha kawaida kumkuta mtoto kama huyu akifanya mambo makubwa, nilimkuta akitengeneza mdundo ambao ulinifanya niupende hivyo ninaamini mdundo huo nitautumia katika moja ya kazi zangu ili niweze kumkumbuka mwanangu,” aliandika Swizz Beatz kwenye akaunti yake ya Instagram.