Azam tv kusaka vipaji vipya leo Coco Beach

0
670

Azam NatashaNA BADI MCHOMOLO

KITUO cha Televisheni cha Azam kupitia channel yake ya Sinema zetu, kinatarajia kuvumbua vipaji vya wasanii chipukizi kupitia mpango wao mpya ujulikanao kama ‘Kiwanda cha Filamu’.

Msimamizi wa Uzalishaji wa Sinema zetu kupitia Channel 103, Zamaradi Nzowa, alisema mradi huo ulianza tangu mwanzoni mwa Machi mwaka huu kupitia mitandao ya jamii.

Na leo wanatarajia kufanya mchujo kwa waliotuma kazi zao kupitia mitandao hiyo na usaili huo unatarajia kufanyika eneo la Coco Beach jijini Dar es Salaam, kuanzia saa 3:00 asubuhi.

Washiriki zaidi ya 200 walituma kazi zao na chipukizi 20 wanatarajiwa kupatikana kwa ajili ya kushiriki filamu hiyo mpya ya ‘Taxi’.

“Usaili huo utakuwa wa siku nne ambao utaanza kesho (leo) katika ufukwe wa Coco, wakisimamiwa na majaji wawili ambao ni msanii nguli, Susan Lewis (Natasha) pamoja na Issa Mbura aliyepata umaarufu sana katika filamu ya Home Coming,” alisema Zamaradi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here