29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kim asimamia zoezi la urushaji makombora Korea Kaskazini

PYONGYANG, KOREA KASKAZINI

SERIKALI ya Korea Kaskazini imethibitisha kuwa Rais Kim Jong-un ameongoza mwenyewe majaribio ya makombora kadhaa ya masafa ya kati na marefu.

Hii ni mara ya kwanza kwa taifa hili kuendesha majaribio hayo tangu mwaka 2017, ikiwa ni matokeo ya juhudi zilizoongozwa na Rais wa Marekani Donald Trump kujenga uhusiano na taifa hilo.

Kim alito igizo la kurushwa makombora ili kuimarisha uwezo wa kujihami wa taifa, lilisema shirika la taifa la habari la nchi hiyo (KCNA).

Rais Trump aliandika katika mtandao wake wa Twitter kuwa anaamini Kim hawezi kuvuruga uhusiano wao pamoja hatua waliyofikia katika harakati za kuleta usalama katika rasi ya Korea.

Aliongeza; “Kim anajua kuwa anaweza kunitegemea kwa hili na kwamba katu hatavunja ahadi yake kwangu. Muafaka utapatikan!

“Naamini Kim Jong-Un anaufahamu fika uwezo wa kiuchumi wa Korea Kaskazini na hatafanya lolote baya kudidimiza matumaini hayo,” Trump aliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Februari mwaka huu mkutano wa Hanoi kati ya Rais wa Marekani, Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ulimalizika bila kufikia makubaliano baada ya Marekani kukataa kutoa nafuu ya vikwazo kwa Korea Kaskazini.

Ripoti yake ya jana, KCNA ilisema kuwa Kim amesisitiza umuhimu wa kulinda ustawi wa kisiasa na kiuchumi wakati nchi inapokabiliwa na hatari ya kuvamiwa.

Lengo la kufanyia majaribio silaha hizo lilikuwa ni kukagua uwezo wake na jinsi zinavyofanya kazi ,” ilisema taarifa hiyo.

Rais wa Korea Kaskazini aliwaambia wanajeshi wake kuwa amani na usalama wa uhakika unahakikishwa kupitia uwezo wa kujilinda”.

Inaaminika hatua ya Korea Kaskazini kufanyia majaribio silaha zake inalenga kuishurutisha Washington kuendelea mbele na mazungumzo ya nyuklia

Katika taarifa ya pamoja wakuu wa usalama nchini Korea Kusini wamethibitisha Korea Kaskazini ilirusha makombora ya masafa mafupi kutoka rasi yake ya Hodo karibu na pwani ya mashariki ya Wonsan hadi Kaskazini Mashariki

Makombora hayo yaliruka kati ya kilomita 70 hadi 200 kabla ya kuanguka katika Bahari ya Japan, waliongeza.

Seoul inasema kuwa iliwahi kuiomba Pyongyang kusitisha shughuli zake kwa sababu zitazua hali ya taharuki katika rasi ya Korea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles